Friday, May 18, 2012

FURAHA YA MOYO WANGU

MAITI INAYOTEMBEA (WALKING CORPSE)

Baada ya khojiwa na wale maafisa wa usalama, Precious (Shanice) alihakikishiwa kuwa wazazi wake watakuwa sawa kwa sababu tayari jitihada za kidiplomasia zilikuwa zikifanywa kati ya ubalozi wa Tanzania na serikali ya nchi hiyo. Kwa sababu kulikuwa na uhusiano mzuri wa kibalozi ati ya nchi hizo mbili, alihakikishiawa kuwa wazawi wake watakuwa salama na watarejea salama.

Taarifa ile ilikuwa njema sana kwa Precious (Shanice) na ilimuongezea nguvu za kupona haraka. Aliendelea kutibiwa ili kumaliza kabisa sumu ya madawa ya kulevya iliyokuwa ndani ya mwili wake. Wakati madaktari wakiendelea kumtibu, walibaini tatizo lingine.

Wednesday, May 16, 2012

OOH MKE WANGU!

Mwangwi wa vilio na simanzi kutoka kwa watu waliopoteza maisha baada ya meli kuzama kwenye mkondo wa bahari wa Nungwi, Zanzibar uliambaa kwenye maji na kwenda kugota kwenye ukuta wa chini ya bahari, mahali palipokuwa na maelfu ya makaburi yalichongwa kwenye mwamba mgumu kuhitimisha safari ya wote waliopoteza maisha yao kwenye ajali hiyo ya kihistoria.
 Kwa binadamu wa kawaida, wenye macho yanayoweza kutofautisha giza na mwanga pekee, hiyo ilikuwa ni ajali ya bahati mbaya kama zilivyo ajali nyingine lakini kwa wale wenye uwezo wa kuona zaidi  ya upeo wa  kawaida wa binadamu (beyond normal vision), haikuwa ajali ya bahati mbaya bali kitu kikubwa zaidi kilichopangwa na kuratibiwa kwa umakini wa hali ya juu.

Friday, May 4, 2012

MAKABURI YA NUNGWI

“Babu! Mbona nasikia vilio vya watu wengi sana! Kwani kuna nini?” kijana mdogo anayefundishwa imani za kishirikina, Kahungo alikuwa akimuuliza babu yake.
“Hivyo ni vilio vya roho zilizopokonywa miili yao bila kujiaanda.“
“Unamaanisha nini babu?”