Baada ya khojiwa na wale maafisa wa usalama,
Precious (Shanice) alihakikishiwa kuwa wazazi wake watakuwa sawa kwa sababu
tayari jitihada za kidiplomasia zilikuwa zikifanywa kati ya ubalozi wa Tanzania
na serikali ya nchi hiyo. Kwa sababu kulikuwa na uhusiano mzuri wa
kibalozi ati ya nchi hizo mbili, alihakikishiawa kuwa wazawi wake watakuwa
salama na watarejea salama.
Taarifa ile ilikuwa njema sana kwa Precious
(Shanice) na ilimuongezea nguvu za kupona haraka. Aliendelea kutibiwa ili
kumaliza kabisa sumu ya madawa ya kulevya iliyokuwa ndani ya mwili wake. Wakati
madaktari wakiendelea kumtibu, walibaini tatizo lingine.
Binti kabla ya kupata na tatizo hii ulikua
unatumia kilevi gani?”
Akuu, mi situmii kilevi chochote.
“Hunywi pombe au kuvuta sigara?
“Wala, sijawahi hata siku moja.”
“Binti sema ukweli ili tukusaidie kwani
tumebaini tatizo katika mfumo wako wa damu.”
“Dokta mbona unanilazimisha nikubali kitu
ambacho sijawhai kukifanya?” aling’aka Shanice. Kwa kuwa daktari alikuwa mtu
mzima na mwenye uzoefu wa kutosha kwenye fani yake ya utabibu, aliamua kutumia
mbinu kali ili kupata ukweli kama Shanice alishakuwa ameanza kutumia madawa ya
kulevya kabla ya siku ya tukio.
Alimtishia kuwa kuna dawa anataka kumpa lakini
inatakiwa itumiwe na mtu ambaye hajawahi kunywa, pombe, kuvuta sigara au
kutumia madawa yoyote ya kulevya. Akawambia kama alishawahi kufanya kimoja kati
ya vitu hivyo, ni bora asema mapema kwani asiposema, endapo dawa ile ikianz
kufanya kazi, uwezekano mkubwa ni kwamba atakufa.
“Unaniruhusu niendelee?” alisema daktari huu
akivuta dawa kutoka kwenye kichupa kidogo kwa kutumia sindano. Maelezo yale
yalimtisha sana Sahnice, ikabidi aseme ukweli.
“Dokta subiri kwanza, ukweli ni kwamba niliwahi
kutuia madawa ya kulevya na kunywa pombe, naomba nibadilishie dawa nisije
nikafa.”
Daktari alishusha pumzi ndefu baada ya kuupata
ukweli.
“”Ilikuaje binti mdogo kama wewe uanze
kujihusisha na mambo hatari kama matumizi ya dawa za kulevya?”
“Ni rafiki yangu alinishawishi.”
Wazazi wako wanajua?”
“Hapana hawajui chochote, nakuomba hata Mungu
akiwasaidia wakarudi salama usiwaambnie kitu chochote,” alijitetea Shanice huku
akigeukia ukutani kwa aibu. Daktari alimuahidi kuwa atamtunzia siri ilr lakini
akaanza kwanza kumpa ushauri nasaha juu ya athari za madawa ya kulevya kwatika
mwili wa binadamu. Alitumia muda mrefu kumuelewesha mpaka alipoona somo
imemuingia kichwani.
“Niahidi kama hutarudia tena.”
“Nitajitahidi dokta lakini kuna muda mwingine
nakuwa nashindwa kuvumilia.”
“Hiyo ni hali ya kawaida, itabidi uunganishwe katika
tiba maalum iitwayo Rehabilitation na kwa sababu bado hayajakuathiri sana,
uwezekano wa kupona ni mkubwa,” alisema daktari, wakakubaliana ambapo
alimalizia kumpa dawa shanice kisha akamuacha apumzike.
***
Baada ya kukamatwa na polisi, Papaa Masafa akiwa
njiani kupelekwa kituoni, aliendelea kuwashawishi wale polisi wakubaliane na
ombi lake la kuuachilia huru kwa ahadi tamu kuwa atawalipa kiwango kikiubwa cha
fedha kama shukrani. Licha ya awali kuonesha msimamo wa hali ya juu, wale
polisi walianza kukonyezana na kupeana ishara juu ya nini cha kufanya baada ya
kutangaziwa dau nono.
“Sikia broo, we twende kwanza kituoni
tukaonekane kama tumetekeleza maagizo ya wakubwa wetu kisha mambo mengine
yatafuatia,” alisema kiongozi wa msafara ule kwa sauti ya kunong’ona. Papaa
Masafa aliomba kupea simu ili azungumze na vijana wake waliokuwa nchin
Pakistan. Wale polisi walimruhusu, akaanza kuongea na upande wa pili wa simu.
Kwa kuwa alikuwa akitumia lugha ya
kiarabu, hakuna aliyeelewa. Akawa anawapa maeleezo vijana wake kuwa wanawake
watatu ambao walikuwa tayari wameshauliwa na kupakiwa kiwango kikubwa cha
madawa ya kulevya, wasafirishwe haraka kuja Tanzania lakini akaonya kuwa
wasipitishwe kwenye uwanja wa ndege wa Dar es Salaam na badala yake wapelekwe
mpaka Lusaka< Zambia kisha wataingizwa nchini kwa kutumia barabara.
Aliwasisitiza kuwa Mzee Kibacha namkewe
wasidhuriwe kwani tayari siri ilishafichuika nchini Tanzania. Upande wa pili
ukamjibu kuwa hali ilikuwa mbaya zaidi kwao ka sababu wanajeshi wa Pakistan walikuwa
wameizingira hospitali Balochistan Kashmir na kwamba uwezekano wa kutoroka
ulikuwa mdogo.
“Tumieni njia ya handaki la chini ya ardhi
kuwatorosha hao wengine ambao mmeshapaki mzigo kwenye miili yao vinginevyo
mtakuwa mmesababisha hasara kubwa sana,” alisema kwa mamlaka kisha akakata
simu. Taarifa kuwa hospitali yake nayo ilikuwa imezingirwa na polisi zilizidi
kumchanganya Papaa Masafa, akawa anaongea peke yake kama mwendawazimu. Hakutaka
kuamini kuwa mipango yake yote ingekwama kirahisi namna ile.
No comments:
Post a Comment