Do you like horror and heart-felt stories? Here is the only place you can get and read them for free. Join our family...
Friday, May 18, 2012
MAITI INAYOTEMBEA (WALKING CORPSE)
Baada ya khojiwa na wale maafisa wa usalama,
Precious (Shanice) alihakikishiwa kuwa wazazi wake watakuwa sawa kwa sababu
tayari jitihada za kidiplomasia zilikuwa zikifanywa kati ya ubalozi wa Tanzania
na serikali ya nchi hiyo. Kwa sababu kulikuwa na uhusiano mzuri wa
kibalozi ati ya nchi hizo mbili, alihakikishiawa kuwa wazawi wake watakuwa
salama na watarejea salama.
Taarifa ile ilikuwa njema sana kwa Precious
(Shanice) na ilimuongezea nguvu za kupona haraka. Aliendelea kutibiwa ili
kumaliza kabisa sumu ya madawa ya kulevya iliyokuwa ndani ya mwili wake. Wakati
madaktari wakiendelea kumtibu, walibaini tatizo lingine.
Wednesday, May 16, 2012
OOH MKE WANGU!
Mwangwi wa vilio na simanzi kutoka kwa watu waliopoteza
maisha baada ya meli kuzama kwenye mkondo wa bahari wa Nungwi, Zanzibar
uliambaa kwenye maji na kwenda kugota kwenye ukuta wa chini ya bahari, mahali
palipokuwa na maelfu ya makaburi yalichongwa kwenye mwamba mgumu kuhitimisha
safari ya wote waliopoteza maisha yao kwenye ajali hiyo ya kihistoria.
Kwa binadamu wa
kawaida, wenye macho yanayoweza kutofautisha giza na mwanga pekee, hiyo ilikuwa
ni ajali ya bahati mbaya kama zilivyo ajali nyingine lakini kwa wale wenye
uwezo wa kuona zaidi ya upeo wa kawaida wa binadamu (beyond normal vision),
haikuwa ajali ya bahati mbaya bali kitu kikubwa zaidi kilichopangwa na
kuratibiwa kwa umakini wa hali ya juu.
Friday, May 4, 2012
MAKABURI YA NUNGWI
Mwangwi wa
vilio na simanzi kutoka kwa watu waliopoteza maisha baada ya meli kuzama kwenye
mkondo wa bahari wa Nungwi, Zanzibar uliambaa kwenye maji na kwenda kugota
kwenye ukuta wa chini ya bahari, mahali palipokuwa na maelfu ya makaburi
yalichongwa kwenye mwamba mgumu kuhitimisha safari ya wote waliopoteza maisha yao
kwenye ajali hiyo ya kihistoria.
Kwa binadamu wa kawaida, wenye macho yanayoweza
kutofautisha giza na mwanga pekee, hiyo ilikuwa ni ajali ya bahati mbaya kama
zilivyo ajali nyingine lakini kwa wale wenye uwezo wa kuona zaidi ya upeo wa kawaida wa binadamu (beyond normal vision),
haikuwa ajali ya bahati mbaya bali kitu kikubwa zaidi kilichopangwa na
kuratibiwa kwa umakini wa hali ya juu.
“Babu! Mbona
nasikia vilio vya watu wengi sana!
Kwani kuna nini?” kijana mdogo anayefundishwa imani za kishirikina, Kahungo alikuwa
akimuuliza babu yake.
“Hivyo ni vilio
vya roho zilizopokonywa miili yao
bila kujiaanda.“
“Unamaanisha nini
babu?”
Subscribe to:
Posts (Atom)